3 Desemba 2013 - 20:30
Russia kamwe haitapambana na Marekani

Rais Putin ameyasema hayo alipojadiliana na wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu maana ya mkakati wa kijeshi wa Ncha ya Kaskazini kwa Russia.

Rais Putin ameyasema hayo alipojadiliana na wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu maana ya mkakati wa kijeshi wa Ncha ya Kaskazini kwa Russia. Amesema Russia haipendi kuona hali ya eneo hilo inazidi kuwa mbaya, na kamwe haitapambana na nchi husika ikiwemo Marekani, na badala yake inatarajia kuendeleza uhusiano wa kiwenzi kati yao.

Rais Putin amesema Ncha ya Kaskazini si kama tu ina maslahi makubwa ya kiuchumi kwa Russia, bali pia ni sehemu muhimu ya kuonesha uwezo wa kujilinda wa nchi hiyo.